Add parallel Print Page Options

Hivyo tunayaeleza makanisa mengine ya Mungu namna tunavyojivuna kuhusu ninyi. Tunawaeleza jinsi mlivyoendelea kwa subira kuwa imara na waaminifu, ingawa mnateswa na kusumbuliwa na matatizo mengi.

Mungu Atafanya Mambo Kuwa Sawa

Huu ni uthibitisho kwamba Mungu ni wa haki katika hukumu zake. Hutaka kuwastahilisha katika ufalme wake. Kuteswa kwenu ni kwa ajili ya ufalme huo. Ni haki kwa Mungu kuwaadhibu wale wanaowaletea matatizo.

Read full chapter